MWANASOKA mkongwe kutoka Ivory Coast Didier Drogba ametoa hospitali yake kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona nchini humo.

Mwanasoka huyo ameikabidhi serikali hospitali yake inayoitwa Laurent Pokou ili kusaidia katika matibabu ya wagonjwa wa Corona

Hospitali hiyo ipo katika jiji la biashara nchini humo, Abidjan pia mpaka kufikia saa ishirini na nne zilizopita Ivory Coast imeripoti vifo vya watu wanne vilivyotokana na ugonjwa wa corona huku maambukizi yakifikia watu 533

Mkuu wa Mkoa Bw Vicent Toh Bi Irie amemshukuru mwanasoka huyo kwa msaada alioutoa kwa nchi yake,

“Tunamshukuru Drogba kwa zawadi aliyoitoa, ni kitendo cha uzalendo Toh Bi alisema.

Didier Drogba aliipa hospitali hiyo jina la Laurent Pokou ili kutoa heshima kwa mwanasoka wa zamani wa Ivory Coast aliyeitwa Laurent Pokou.

Didier Drogba ametoa hospitali yake kwa ajili ya kusaidia matibabu ya wagonjwa wa corona Ivory Coast.