NYOTA wa muziki wa kizazi kipya Harmonize amemtambulisha msanii mpya ambaye amesaini chini ya lebo yake inayojulikana kwa jina la Konde Music Worldwide kama msanii ambaye atafanya kazi yake akiwa chini ya lebo hiyo.

Mwanamuziki huyo anayetamba kwa wimbo wa Bedroom kupitia ukurasa wake wa instagram amemtambulisha msanii huyo anayekwenda kwa jina la Ibraah_tz.

“Kipaji, uwezo wako, na aina ya kufikiri vinanifanya nikuone kama pacha wangu,… Mungu amekupatia na Watanzania wapotayari kukupokea, all the best bro”

aliandika Harmonize

Pia Harmonize ametumia nafasi hiyo kuwashukuru Watanzania wote ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kufanya muziki wake ukue kwa kasi na kuleta mafanikio makubwa kwake na katika tasnia ya muziki Tanzania.

Hivi karibuni Harmonize aliachia albamu yake inayokwenda kwa jina la AFROEAST ambayo mpaka sasa inafanya vizuri katika tasnia ya muziki Afrika kwa kushika nafasi mbalimbali ikiwemo audiomack charts Afrika ambapo albamu hiyo ilishika nafasi ya saba.