Mchekeshaji Edward Hugh McGinnis maarufu kama Eddie Large amefariki dunia tarehe 2 mwezi Aprili kwa ugonjwa wa Corona akiwa na umri wa miaka 78, Eddie amekuwa maarufu kwa uchekeshaji kati ya miaka ya 1970 mpaka 1980 akishirikiana na mchekeshaji mwenzake Syd Little.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na familia yake kupitia ukurasa wa Facebok, familia yake imeandika kuwa, kabla ya kufariki Eddie kufariki kwa ugonjwa wa corona, alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kushindwa kufanya kazi kwa muda mrefu,

Aidha Syd Little, rafiki wa karibu wa marehemu ameiambia BBC kuwa “kwa muda mrefu tumekuwa marafiki, tutamkumbuka daima, tunajivunia kila jambo jema ambalo amelifanya hapa duniani”

Familia ya marehemu imesema kuwa bado haijaruhusiwa kwenda kuaga mwili wa marehemu huko hospitali kutokana na vizuizi vilivyoweka kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa corona