Ugonjwa wa Corona wazidi kuitikisa Rwanda baada ya Serikali hiyo kuongeza muda wa kutotoka nje mpaka ifikapo tarehe 19 Aprili

Serikali ya Rwanda imeongeza muda wa marufuku ya kutotoka nje kwa raia wake mpaka hapo ifikapo Aprili 19, Marufuku hiyo imefuatiwa na ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona kutoka watu 17 mpaka 82 kwa takribani majuma mawili yaliyopita.

What are your views upon corona virus outbreak, will it reverse globalization?

Imeelezwa kuwa Baraza la Mawaziri nchini Rwanda limetoa ruhusa ya kutoka nje endapo raia wake atakuwa akienda kununua chakula au dawa tu na si vinginevyo, pia serikali ya Rwanda imewasambaza askari wake ili kuhakikisha sheria hiyo inatekelezwa.

Aidha Baraza limetangaza kuwa wakati huu wa muda wa nyongeza mipaka itakuwa inafungwa na mizigo na raia wa Rwanda pekee ndio watakaoruhusiwa kuingia nchini humo

Pia waajiriwa watatakiwa kufanya kazi wakiwa majumbani mwao huku shule zikishauriwa kutumia teknolojia katika kutoa maelekezo ya masomo

Processing…
Success! You're on the list.