HABARI

Burundi yathibitisha wagonjwa wa Corona kwa mara ya kwanza

Burundi yathibitisha kuwa na wagonjwa wawili wa corona kwa mara ya kwanza.

BBC swahili

WAZIRI wa afya wa Burundi Thadee Ndikumana, ametangaza watu wawili ambao ni raia wa burundi kuwa na maambukizi ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona.

Aidha Waziri Ndikumana amesema kuwa, Raia hao wote ni wanaume, mmoja ana umri wa miaka 56 na mwingine umri wa miaka 42, na walikuwa wakiwasili nchini Burundi kutokea Dubai wakiptia Rwanda.

Akiongea na BBC siku kadhaa zilizopita, msemaji wa Rais wa Burundi Bwana Jean Claude Karerwa alisema kuwa “Mungu atawalinda na maambukizi haya kwa sababu Mungu ameiweka serikali ya Burundi katika sehemu ya Kipekee”

Lakini maambukizi haya yameikumba Burundi huku ikiwa inatarajia kuwa na uchaguzi mkuu ifikapo tarehe 20 Mei, Bwana Karerwa aliongeza kuwa mabadiliko ya kufanywa kwa uchanguzi yanaweza kutokea endapo ugonjwa huu utaingia na kushambulia Burundi kwa kiasi kikubwa sana.

 

 

Categories: HABARI

Tagged as: ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.