Share the Article on social media

“SHIRIKA la Afya duniani WHO limeeleza jitihada mpya katika kukabiliana na virusi vya corona”

Kufikia tarehe 23, 2020 zaidi ya maambukizi 350,000 yameripotiwa kutoka katika mataifa 170 duniani kote, huku watu 16,000 wakipoteza maisha, idadi hiyo inaonekana kuongezeka kila uchao.

“Kuukabili ugonjwa wa corona kwa kuishi katika vizuizi bila ya kuwa na chanjo ama tiba bado itakuwa ni ndoto tu” kwasababu hiyo Shirika la Afya duniani WHO limeanzisha mpango wa mshikamano “solidarity”, ambapo mataifa kumi yatahusika katika kufanya majaribio ya dawa nne ambazo hutumika kukabiliana na magojwa mengine jinsi zitakavyoweza kutibu ama kuzuia makali ya ugonjwa wa corona.

Shirika la afya duniani limeeleza kuwa lengo la mpango huo ni kuhakikisha dawa ya kutibu virusi vya corona inapatikana mapema, ukilinganisha na mchakato wa kutengeneza dawa mpya ambao utachukua miaka kadhaa ili kukamilika.

Argentina, Canada, Afrika Kusini, Bahrain, Ufaransa, Iran, Norway, Uhispania, Switzerland na Thailand ni mataifa ambayo yamejiunga katika utafiti wa tiba itakayotibu ama kupunguza makali ya Corona

JE mpango wa WHO kushirikisha mataifa kumi duniani katika kutafuta tiba ya ugonjwa wa corona unaweza kuharakisha upatikanaji wa tiba hiyo?

CLICK TO TWEET

“Umuhimu wa utafiti kama huu ni kwamba unaweza kusajili wagonjwa wengi kwa haraka” alisema daktari George Rutherford ‘Profesa wa takwimu za kibailojia katika chuo kikuu cha Carlifonia nchini Marekani.

“Iwapo kwa mfano nilikuwa nikifanyia majaribo katika maabara yangu ningekuwa na wagonjwa wawili au watatu kwa siku, lakini kutokana na ushirikiano huu unaweza kuwa na wagonjwa 100 kwa siku” aliongeza Dk. George Rutherford.


Jopo la wataalamu kutoka Shirika la Afya duniani limechagua tiba nne zenye dawa mchanganyiko ambazo zimetumika kutibu Ebola, Malaria, pamoja na HIV, ili kuzifanyia majaribio ya kutibu virusi vya corona. (TAHADHARI: BADO DAWA HIZI HAZIJATHIBITISHWA KWA MATUMIZI)

  1. REMDESIVIR

Dawa hii ilitengenezwa kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa Ebola, hivi karibuni imeonekana kuwa na uwezo dhidi ya virusi vya corona kulingana na vipimo vya seli zilizopandwa katika maabara.

Hata hivyo kumekuwa na ripoti kwamba dawa hii imekuwa na matokeo chanya kwa wagojwa wa COVID-19, lakini bado shirika la afya duniani limesema kuwa haitoshi kuthibitisha dawa hii inaweza kutumiwa katika kutibu ugonjwa huo.

Steven Morse, Mkurugenzi wa magonjwa ya kuambukiza chuo kikuu cha Columbia (EE) aliambia BBC, kuwa Kati ya dawa zilizojumuishwa katika mpango wa solidarity redemsivir “inaonekana kuwa na uwezo mkubwa katika kukabiliana na virusi vya corona katika vipimo vya maabara”

    2. CLOROQUINE/HIDROXICLOROQUINE

Dawa hii ilitumika miaka mingi iliyopita kutibu ugojwa wa maralia, daktari Rutherford anasema kuwa itakapotumiwa na mgonjwa basi huweza kusababisha maudhi kama vile kukosa hamu ya kula, kuhara, maumiu ya kichwa, kuapata vipele katika ngozi na kutapika kulingana na utafiti uliofanywa na Maktaba ya Kitaifa ya Tiba nchini Marekani,

Hata hivyo iwapo inaweza kutibu malaria haimaanishi inaweza kufanya kazi dhidi ya virusi vya corona aliongeza daktari Rutherford.

   3. RITONAVIR NA LOPINAVIR

Mchanganyiko wa dawa hivi umekuwa ukitumika katika matibabu ya ugonjwa wa HIV hata hivyo dawa hii imeonekana kutoleta matumaini katika kutibu virusi vya corona,

“lakini ni busara kujaribu tena” alisema daktari Rutherford

   4. RITONAVIR AU LIPONAVIR

Tiba ya nne kupimwa na Shirika la afya duniani ni mchanganyiko wa dawa hizi pamoja na interferon-beta, molekyuli ambayo husaidia kudhibiti uchochezi kwa wanyama ambao wameambukizwa ugonjwa wa kupumua katika Mashariki ya Kati (MERS),

Wataalamu wanaonya kuwa ni muhimu kuwa makini katika matumizi ya mchanganyiko huu kwani unapotumika katika hatua za mwisho mwisho basi huweza kukosa ufanisi na kusababisha madhara kwa mgonjwa.