MCHUNGAJI maarufu kutoka Nigeria, TB Joshua hivi karibuni amekuwa miongoni mwa watumishi wa Mungu waliotoa utabiri kuhusu janga la virusi vya Corona.

TB Joshua ametabiri janga la virusi vya Corona litaisha Machi 27, 2020.

Video fupi iliyosambaa mitandaoni imemuonyesha mchungaji huyo akiwa anahubiri kuhusu virusi vya Corona na kusema kuwa “kama ugonjwa huu haukuletwa kwa dawa, basi dawa haziwezi kuuondoa”

Leo Machi 28 wanaigeria wamshambulia mchungaji huyo kwa maneno kupitia mitandao ya kijamii wakisema kuwa “Mpaka sasa tarehe hiyo imeshafika lakini bado janga hilo linaendelea kuitikisa Nigeria na dunia kwa ujumla”.

https://platform.twitter.com/widgets.js“>

Baadhi ya maneno yaliyochapishwa na Wanigeria kupitia mtando wa twitter kuhusu utabiri wa TB Joshua.