HAKUNA kusubiri tena! Nyota wa muziki wa Pop na R&B nchini Marekani Rihanna Fenty amesikika kwa mara ya kwanza baada ya ukimya wa muda mrefu katika kolabo aliyoshirikishwa na PARTNEXTDOOR katika ngoma iliyoenda kwa jina la “Believe it”

Nyota huyo ambaye alitangaza kuachia albamu yake hivi karibuni amesikika akiimba kiitikio katika nyimbo mojawapo katika albamu ya PARTNEXTDOOR ambayo ameiachia leo hii tarehe 27 Machi, hali iliyofanya mashabiki wa RiRi kuwa na furaha kuisikia sauti ya mkongwe huyo katika kipindi hiki ambako duniani inapambana vita dhidi ya Corona .

Katika nyimbo hiyo PND ameonekana akiomba msamaha kwa mpenzi wake huku rihanna akirudia kiitikio “That’s when you believe it/ That’s when you believe it/ Believe when you see it.” Mashabiki wa Rihanna wameonekana kustaajabishwa na ujio wa Rihanna katika nyimbo hiyo baadhi yao wameweka jumbe zao katika mtandao wa twitter zilizosomeka kuwa “PARTNEXTDOOR AMEACHIA ALBAMU!! NA RIHANNA YUPO KWENYE ALBAMU!! NARUDIA RIHANNA YUPO KWENYE ALBAMU!” shabiki wa Rihanna aliandika.

Nyimbo ya “Believe it” imewarudisha upya Rihanna pamoja na PND katika ramani ya muziki Marekani na dunia nzima kwani tangu kuachiwa kwa albamu ya PND ya mwaka 2016 iliyoitwa Party next door hakuwahi kutoa albamu nyingine tena.

https://open.spotify.com/embed?uri=spotify%3Aalbum%3A2T8UlI17u5hwTqu6zkpkW7” target=”_blank” rel=”noopener”>ALBAMU YA PARTNEXTDOOR

Ikumbukwe kuwa PND aliwahi kushiriki katika albamu ya mwisho ya Rihanna iliyokwenda kwa jina la ANTI, huku akihusishwa katika utunzi wa baadhi ya nyimbo kama vile “Work” ya Rihanna na Drake pia “Sex with Me”. Muunganiko wa nyota hawa wawili ulirudishwa tena na Dj Khaled katika ngoma ya “Wild Thoughts”.