TAIFA la Marekani imethibishwa kuwa na kesi nyingi zinazotokana maambukizi ya virusi vya Corona kuliko taifa lolote duniani, mpaka sasa Marekani imeripotiwa kuwa na maambukizi 85,500.

Shirika la BBC limeripoti kuwa “kwa mujibu wa takwimu za sasa zilizokusanywa na Chuo Kikuu cha John Hopkins, Marekani imeripotiwa kuwa na maambukizi mengi zaidi ya Italia yenye maambukizi 80,589 na China yenye maambukizi 81,782.

Aidha vifo 1,300 vilivyotokana na ugonjwa wa Corona vimeripotiwa nchini Marekani, hali inayoifanya Marekani kuwa na idadi ndogo zaidi ya Italia yenye vifo 8,215 na China yenye vifo 3,291.

Idadi kubwa ya maambukizi imekuja kipindi ambacho Rais Trump akitegemea kuwa hali itaanza kuwa shwari muda i mrefu.

Pia makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence amesema kuwa vipimo vya virus vya corona vipo katika kila jimbo nchini Marekani ambapo mpaka sasa tayari wameshapima kufikia idadi ya watu 552,000.