WAKATI dunia ikiwa macho kupambana na virusi vya Corona, vifo vitokanavyo na ugonjwa huo vimeongezeka zaidi Uhispania na kulifanya taifa hilo kuwa nafasi ya pili kwa idadi kubwa ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo duniani.

Shirika la habari BBC limeripoti kwa Idadi ya watu waliofariki na ugonjwa huo nchini Uhispania imeongezeka hadi kufikia 738 ndani ya saa 24 kila siku mpaka kufikia zaidi ya vifo 3,434 ambayo ni idadi kubwa kuwahi kuripotiwa baada ya Italia.

Hadi kufikia sasa Italia inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Corona huku idadi yake ikiwa ni 7,503 ikifuatiwa na Uhispania yenye vifo 3,434 na China 3,285.

Licha ya jitihada zilizowekwa na viongozi wa nchi mbalimbali  katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona bado maambukizi yanaendelea kuwa makubwa katika baadhi ya nchi za Ulaya

Wakati huohuo Marekani imeripoti idadi ya visa vya ugonjwa huo kufikia 70,000 huku vifo vitokanavyo na maambukizi hayo kufikia 1,050. idadi ya maambukizi imeonekana kuongezeka hadi kufikia 10,000 kwa siku moja.