RAIS wa Marekani, Donald Trump aanaamini kuwa dawa aina ya Hydrochloroquine na Azithromicin zinaweza kutumika katika kutibu ugonjwa wa COVID-19 katika mwili wa binadamu.

Takribani wiki moja Rais Trump amekuwa akisisItiza majaribio ya dawa hizo kufanyika kwa haraka chini ya idara ya chakula na dawa (FDA) Marekani.

Akizungumza na wanahabari nchini Marekani Rais Trump alisema kuwa

“Inaaminika kuwa na matumaini baada ya kutoa matokeo mazuri, na tunahakikisha kuwa dawa hiyo inapatikana kila mahli mara moja”

“Nafikiria inaweza ikaleta manufaa na pengine hata kushindwa lakini nadhani inaweza, kutokana na kile nachoona inaweza kubadilisha mambo.. Dawa hii ina uwezo mkubwa, ina uwezo mkubwa” Rais Trump aliongezea.

Aidha siku ya jumamosi Rais Trump alisisitiza zaidi kupitia katika ukurasa wake wa Twitter akiandika kuwa,  “Hdyroxychroloquine na Azithromycin  zikitumika kwa pamoja zinaweza kuleta manufaa makubwa katika historia ya tiba, FDA imefanya kitu muhimu. Asanteni ni matumaini kuwa (H hufanya kazi vizuri ikiwa na A International Journal of Antimicrobial Agents.)”

Hapo awali Rais Trump alisema kuwa tayari dawa hiyo imeshaidhinishwa na idara ya chakula na dawa FDA kwa matumizi kwa kuwa ni maarufu na rahisi kutengenezwa.

Hata hivyo Kamishna wa FDA nchini Marekani, Stephen Hahn amekanusha taarifa hizo za kuidhinishwa kwa matumizi ya dawa hizo dhidi ya ugonjwa wa Corona, huku akisema kuwa dawa hizo bado zinafanyiwa majaribio katika maabara za FDA hivyo matumizi dhidi ya COVID-19 bado hayajaruhusiwa.

Ikumbukwe kuwa dawa aina ya Hydrochroloquine ni dawa ambayo imetumika miongo kadhaa kama tiba ya magonjwa mablimbali ikiwemo Malaria kwa kiwango kikubwa barani Afrika pia yabisi na erythematosus na arheumatoid.