SERIKALI ya Kenya imetangaza kupona kwa mtu wa kwanza aliyeugua ugonjwa wa Corona, huku watu watatu wakiripotiwa zaidi.

Akizungumza katika hotuba kwa Taifa la Kenya, Rais Kenyatta alisema kuwa “hali hii inamanisha kuwa ugonjwa huu unaweza kukabiliwa kabisa”.

Mpaka sasa idadi watu walioambukizwa ugonjwa wa Corona nchini Kenya imefikia 28, huku serikali ikiongeza jitihada katika kutangaza njia sahihi za kukabiliana na janga hilo ikiwemo na kutotoka nje kuanzia Ijumaa Machi 27.

Aidha Rais Kenyatta ametangaza hatua ya kupunguza mshahara wake kwa asilimia 80, huku Mawaziri wake wakifuata nyayo hizo kwa kupunguza mishahara yao kwa asilimia 30 ili kusaidia kupambana na ugonjwa wa Corona.

Licha ya hayo Rais Uhuru ametoa wito wake kwa asasi nyingine za kiserikali kukubali kupunguza mishahara yao kwa wakati huu taifa linakabiriana na janga zito la Corona.

Source BBC SWAHILI.