MSANII wa muziki wa Hip Hop Tanzania, Young Killer amefunguka kwa mara ya kwanza juu ya uhusiano uliopo kati yake na muigizaji wa filamu za Bongo, Jackline Wolper.

Akizungumza katika mahojiano na Bongo 5 msanii huyo ameweka wazi juu ya uhusiano wake na Jackline Wolper kufuatiwa na picha za mahaba alizochapisha katika mtandao wa Instagram ikimuonesha Msodoki akiwa na anambusu Jackline Wolper.

Aidha katika mahojiano hayo Young Killer ameeleza juu ya mwanamke ambaye anapenda kuwa naye katika mahusiano ya kimapenzi, Msodoki ameeleza kuwa mwanamke yeyote ambaye ni mpambanaji, mwenye pesa na malengo ya kimaisha basi anaweza kuwa nae katika mahusiano.

Video ya interview aliyofanyiwa Young Killer kupitia Bongo 5.