Bara la Afrika ndilo bara linalokaliwa na watu weusi kwa idadi kubwa kuliko bara lingine lolote duniani. Ndani yake kuna maajabu mengi yanayoweza kukustaajabisha pindi utakapokuwa ukiyasoma ama kuyasikia mahali popote.

Leo tumekuletea baadhi ya mambo 10 ambayo si rahisi kuyapata mahali pengine popote duniani zaidi ya Afrika tu.

  1. Bara la Afrika ndilo bara la pili kwa kuwa idadi kubwa ya watu, inakadiriwa kuwa na wakazi zaidi ya bilioni moja
  2. Bara la Afrika ndilo lenye jangwa kubwa zaidi duniani, Jangwa la Sahara ambalo linakadiriwa kuwa na ukubwa sawa na nchi ya Marekani.
  3. Maporomoko ya Victoria ndio maporomoko makubwa zaidi Afrika, yana urefu wa futi 355 na upana wa maili moja
  4. Madagascar kisiwa kinachopatikana katika bahari ya Hindi ndicho kisiwa kikubwa zaidi Afrika, pia ni kisiwa cha nne kwa ukubwa duniani.
  5. Takwimu zinaonesha kuwa Afrika ndilo bara lenye joto kali zaidi ya mabara yote duniani.
  6. Sudan ndio nchi kubwa kuliko zote Afrika ( kilomita za mraba 968,000).
  7. Cairo ndio mji mkubwa kuliko yote Afrika, nao unapatika nchi ya Misri.
  8. Mnyama mrefu kuliko wote duniani ni Twiga ambao wanapatikana Afrika,
  9. Mnyama wa ardhini mwenye kasi kuliko wote duniani ni Cheetah ambaye anapatikana barani Afrika.
  10. Chura mkubwa duniani anayejulikana kwa jina la (Goliath Frog) anapatikana barani Afrika katika nchi ya Cameroon, chura huyo anaweza kukua hadi kufikia ukubwa wa futi moja (sentimeta 30.5).