NYOTA wa muziki wa kizazi kipya Rajabu Abdul almaarufu kama Harmonize amekiri kumaliza deni lake alilokuwa akidaiwa na lebo yake ya awali (WCB), akiyaongea hayo katika sherehe ya uzinduzi wa albamu yake mpya iliyokwenda kwa jina la AFROEAST.

Mwanamuziki huyo anayetamba kwa ngoma ya Uno ameyaongea hayo alipokuwa akifanya mahojiano na mtangazaji kutoka Clouds Fm, Diva the Boss. Katika mahojiano hayo Harmonize alisema kuwa

“Ninaushukuru uongozi wangu wa zamani (WCB) na  wa sasa (KONDE GANG) kwa kunivumilia kwani imetumika busara kubwa hadi kumaliza  deni, nimelipa kidogo kidogo kwa kuuza baadhi ya vitu vyangu hadi sasa nimefanikiwa  kulipa deni lote”

Soma Pia Harmonize aanika hadharani kuanzishwa kwa Tandahimba FM

Awali Harmonize alikuwa akidaiwa Shilingi Milioni 600 kama gharama aliyotakiwa kulipa baada ya kuvunja mkataba na lebo ya WCB