Harmonize ameanika hadharani  juu ya mpango wake wa kuanzishwa kwa radio Tandahimba mpaka kufikia mwezi wa tatu mwaka huu, akiyasema hayo kutokea uwanja wa majaliwa wilayani Tandahimba.

“KILAMUNU AVENA KWAO”, msemo ambao msanii wa muziki wa kizazi kipya (bongo flava), Harmonize anapenda sana kuutumia katika machapisho yake mitandaoni,

Usiku wa kuupokea mwaka mpya akiwa katika shoo yake iliyofanyika katika uwanja wa Majaliwa wilayani Tandahimba mkoani Mtwara, Harmonize ameamua kuuthibitishia umma kwa vitendo maana kamili ya msemo huu kwa kutoa ahadi ambazo amesema kuwa zitaanza kukamilika ifikapo tarehe 30 mwezi wa tatu 2020.

moja kati ya ahadi ambazo ziliamsha kelele za shangwe kwa mashabiki wa muziki wake ni kuanzishwa kwa Redio Tandahimba, shangwe hizi ziliambatana na maneno ya Harmonize yenye kuonesha nia juu ya jambo hili,

mpaka kufika tarehe 30 mwezi wa tatu, kutakuwa na Tandahimba Fm hapa, uwezo tunao, vifaa tunavyo, nguvu tunayo. lakini niwaambieni kitu kuanzia leo tarehe moja mwezi wa kwanza 2020 pale hospitali ya wilaya shida ya dawa mwisho leo, kingine niwapongeze sana Tandahimba FC kuchukua  taji Mtwara taarifa zenu nimezipata na kuanzia leo mimi ndio mwenyekiti wa Tandahimba FC, alisema Harmonize.

Screenshot_20200102-001328
Picha iliyochapishwa na msanii Harmonize akionesha nia yake katika kusaidia utoaji wa huduma za afya katika hospitali ya Tandahimba

Baada ya kuachana na rekodi lebo ya WCB mwishoni mwa mwaka 2019, na kuendeleza maisha yake ya kimuziki yeye mwenyewe Harmonize amefanya mambo mengi sana, ijapokuwa ni kwa muda mfupi lakini ameweza kufanikiwa katika kuibrand lebo yake mwenyewe iitwayo KONDE GANG, lakini pia kurudisha fadhila zake kwa mashabiki wa muziki wake.

Ikumbukwe kuwa Harmonize alianza kurudisha fadhila hizi kwa kugawa chakula bure mtaani kupitia mgahawa unaotembea aliouita KONDE BOY MGAHAWA mwanzoni tu baada ya kuachana na lebo ya WCB.

Soma pia Harmonize aanzisha mgahawa unaotembea

Lakini leo hii amefikia hatua ya kutoa babkubwa! kwa mashabiki zake na watu wa nyumbani kwake Tandahimba kwa kuwaletea Redio, lakini pia, dawa za hospitalini na kuifadhili timu ya mpira wa miguu ya Tandahimba FC jambo ambalo linaweza kumuweka Harmonize pahala pazuri  kwa kuongeza upendo na ukaribu zaidi kwa mashabiki wa muziki wake.

***************************