Demi Lovato amethibitisha kutengana na mpenzi wake, ikiwa ni mwezi mmoja tu baada ya kuweka wazi mahusiano yao katika ukurasa wake wa instagram.
Mwanamziki huyo mashuhuri nchini Marekani mwenye umri wa miaka 27, amefunguka juu ya uamuzi wake wa kuachana na mpenzi wake Austin Wilson huku akiwataka mashabiki zake kutorusha maneno makali dhidi ya Austin
Demi alituma ujumbe wa moja kwa moja kwenye akaunti ya Instagram ya shabiki wake ambaye alikuwa akimshutumu Austin kwa maneno mabaya kuwa ndiye chanzo cha kuvunjika kwa mahusiano hayo,
Alimuomba kutotumia lugha chafu kwa Austin, lakini pia akimueleza juu ya wakati mgumu alioupitia mpaka kuachana na mpenzi wake huyo.
Katika ujumbe huo Demi aliandika kuwa “Please don’t go after him, he’s a good guy. Much better than what people see on the outside just because he’s got a lot of tattoos. Breakups are hard for both parties involved. just stay nice and say prayers”

Ujumbe uliotumwa na Demi Lovato kwa shabiki wake
Tamko la Demi Lovato juu ya kutengana na Austin limefuatiwa na kufutwa kwa picha zenye kuonyesha mahaba kati yao huku mikononi mwao Wakiwa wameshikilia maua mekundu maarufu kama “Red rossy”.

Demi Lovato akiwa na Austin enzi za mahusiano yao
Picha hizi zilipigwa kitaalamu na mpiga picha aitwaye Angelo Kritikos ambaye kabla ya kufutwa kwa picha hizo aliruhusu kushare picha hizo katika ukurasa wake wa instagram akionesha furaha yake kwa wapenzi hao
Wawili hawa walianza kuchapisha picha zenye kuonyesha haiba ya mapenzi katika kurasa zao za instagram mwanzoni mwa mwezi Novemba 2019, hata hivyo penzi lao limeonekana kutodumu kwa muda mrefu kwani mpaka sasa Demi Lovato ameamua kutengana na Austin huku akiwa hajaeleza wazi sababu ya kuvunjika kwa penzi lao.
******************************
Categories: HABARI
Good ndgu
LikeLike
Imooooo
LikeLike
Imepita hyo mkuu
LikeLike
Thanks bro
LikeLike
😍😍
LikeLike
Thanks
LikeLike