Toni-Anni mrembo kutoka Jamaika ameshinda taji ya urembo wa dunia huko ExCel London, Uingiereza usiku wa  jana

Ni miaka 25 mfululizo tangu 1993-2019 Jamaika haikuwahi kuonja ladha ya  ushindi katika uwanja wa walimbwende wa dunia.  Leo hii 2019 Mrembo Toni-Ann Singh kutoka Jamaika amevunja rekodi hiyo kwa kutwaa taji ya ulimbwende wa dunia 2019 ikiwa ni toleo la 69 lililofanyika mnamo Disemba 14, 2019, ExCel London huko London, Uingereza.  Baada ya Mrembo Lissa Hanna kutoka Jamaika kutwaa taji hilo kwa mara ya mwisho mwaka 1993.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 23, ambaye pia ni mhitimu wa Chuo Kikuu Jimbo la Florida, ndiye mmiliki halisi wa ukurasa wa warembo Jamaika na Amerika safari yake kufikia urembo wa dunia ilianza pale tu baada ya kutwaa taji la Miss Jamaika 2019. Ushindi wake unakamilisha idadi ya warembo wanne kutoka Jamaika waliowahi kuchukua taji hiyo ya  Miss World kuanzia mwaka 1963, 1976, 1993 na 2019

MAISHA YAKE YA AWALI:

Mrembo Toni-Ann Singh alizaliwa mnamo mwaka 1996, huko Morant Bay, Jamaika Kisha akahamia nchini Marekani na kuishi katika jimbo la Florida  akiwa na umri wa miaka tisa, alihudhuria Chuo Kikuu cha Jimbo la Florida  huko Tallahassee, Florida. ambako alifanikiwa kupata digrii ya masomo ya wanawake na saikolojia.

Uzuri wa mrembo Singh unaakisi kutoka mama yake aitwaye Jahrine Bailey Singh mwenye asili ya Kiafrika-Karibea  kutoka Jamaika pia baba yake ni mwenye asili ya Hindi-Karibea kutoka Jamaika. maisha yake ya awali yametawaliwa na matukio mengi sana yenye kufurahisha pia kuhuzunisha, alipokuwa mdogo alipenda sana kuimba muziki na huo ndio ulitawala ndoto za maisha yake ya baadae, alijiunga katika kwaya ya watoto na kupatiwa mafunzo ya kuimba kitaalamu huko Marekani aliliambia jarida la The Gleaner la Jamaika katika mahojiano maalumu.

Katika jitihada zake za uimbaji wa muziki Singh amewahi kuimba cover ya wimbo wa Whitney Houston uitwao “I have nothing” ambao ndio ulikuwa kivutio kikubwa  kwa mashabiki wake katika jukwaa la walimbwende huko London. Licha kuwa na kipaji na sauti nzuri yenye haiba ya uimbaji, Mrembo Singh kwa sasa amewekeza akili yake katika kuwasaidia watu na jamii kwa ujumla.

Hivi karibuni Mrembo Singh aliweka chapisho katika ukurasa wake wa instagram lililomuonesha yeye na mama yake wakila ice cream, chapisho hilo alioneka pia mrembo Singh akieleza jinsi mama yake alivyopambana katika kufanikisha ndoto zake maishani “i found my true passion in the arms of my mother, who has made every sacrifice necessary to give me opportunity for education and a life she has only been able to dream for herself” she says.  “Nilipata shauku yangu ya kweli mikononi mwa mama yangu, ambaye alijitoa kwa kila lililomlazimu kunipatia elimu na maisha  ambaye ameweza kuyatamani” alisema Singh.

Screenshot_20191215-125847
Toni-Ann akila ice cream na mama yake picha kutoka katika mtandao wa Instagram

SAFARI YA KUTWAA MISS WORLD 2019.

Safari ya kutwaa taji ya Miss world ilianzia nchini mwake Jamaika mwanzoni mwa  2019 ambapo Singh alishindana  katika shindano la Miss Jamaika World 2019 ambapo mwishowe aliibuka kidedea na kushinda taji hilo na hatimaye kupewa nafasi ya kuwakilisha warembo kutoka  Jamaica katika mashindano ya Dunia.

Siku moja akiwa mshindani katika taji ya Miss Jamaika alijibu swali aliloulizwa kuwa  endapo ungechaguliwa kuwa mshindi wa taji ya dunia ya miss Jamaika utaitumiaje heshima ya taji lako katika kutoa mchango chanya katika jamii yako?  Singh alisema kuwa ningeendelea kuwatetea wanawake kila mahali na au bila  taji ya dunia ya miss Jamaika. ningeendelea kutetea wanawake  ninaamini kuwa wanawake ndio damu ya jamii yetu” alisema

Mrembo Singh aliondoka kuelekea London mnamo Novemba 2019, ili kushiriki katika shughuli za utabiri wa awali wa kuwania  taji la Miss world, Singh  aliweza kushinda baada kuwania katika 40 ya model na kushinda shindano la Talanta, ambalo ndilo lilimpa nafasi ya kuingia kwake moja kwa moja kwenye mechi 40 za juu.

Usiku wa fainali ulifanyika Disemba 14 2019,  huko ExCel London ambapo singh aliendelea kuwa kidedea kutoka nafasi  40 za juu na kufikia 12 na kupenya hadi tano bora, ndipo hapo Toni-Ann Sigh alipotangazwa kuwa mshindi wa taji ya ulimbwende wa Dunia huku akifuatiwa na mshindi wa pili ambaye ni  Ophe’ly Mezino wa Ufaransa na nafasi ya mshindi wa tatu ikifuatiwa na Suman Rao wa India.

IMG_20191215_144055
Toni-Anni baada ya kutangazwa kuwa ameshinda taji ya Miss World 2019, picha kutoka katika mtandao wa instagram

Pamoja na ushindi wake Singh amekuwa mwanamke wa nne kuwahi kushinda taji hilo kutokea Jamaika, pia ni mwanamke mweusi wa pili kushinda taji hilo baada ya Agbani Darego aliyekuwa mwanamke wa kwanza mweusi kushinda Taji la Miss world kutokea Nigeria mwaka 2001.

Watu wengi huchagua watu ambao huwa kama ndio kioo katika misingi ya maisha yao hapa duniani hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa mlimbwebde huyo wadunia Toni-Ann Singh.

safari yake ya kuwania taji la Miss world ilichochewa zaidi na mshindi wa zamani wa Jamaika, Terri-Karelle Reid ambaye alikutana nae mwaka 2005 akiwa katika hekaheka za kumpata mrembo katika chama cha Frolida Carribean Association ambapo Terri ndiye alikuwa mwamuzi wa mashindano hayo.

Ndipo hapohapo aliposhawishiwa kujiunga na mashindano ya Dunia ya Miss Jamaika. Japo ilikuwa numu wa upande wake lakini hakusita kuufuata ushawishi alioupata kutoka kwa mlimbwende huyo mkongwe “safari moja huanzisha safari nyingine” baada ya kuanza safari ya kuwania taji ya Miss Jamaika na kushinda, hatimaye amefanikiwa kuibuka kidedea na kuondoka na taji ya Miss World jambo ambalo ni faraja kwake, familia na Taifa kwa ujumla.

“Asante kwa kusoma Chapisho letu Karibu ujiunge nasi kwa kubonyeza kitufe cha Follow ili uwe wa kwanza kupata habari mpya kila zinapopakiwa katika blogu hii”.